0688 821 584 George Kunguz - 1 & Visawe 0688 821 584 George Kunguz - 2 METHALI 1. Akili ni nywele-kila mtu ana zake 2. Mcheza kwao -hutunzwa 3. Asiye uliza-hanaajifunzalo 4. Hakuna marefu – yasiyokuwa na ncha 5. Mkataa pema – pabaya panamuita 6. Asiyesikia la mkuu-huvunjika guu 7. Bandubandu – humaliza gogo 8. Chovyachovya – humaliza buyu la asali 9. Asiyefunzwa na mamaye-hufunzwa na ulimwengu 10. Ndondondo-si chururu 11. Akufukuzaye-hakwambii toka 12. Mungu hamfichi -mnafiki 13. Mchumia juani-hulia kivulini 14. Ahadi -ni deni 15. Akiba – haiozi 16. Damu nzito-kuliko maji 17. Siri ya mtungi-aijuaye kata 18. Kupotea njia-ndio kujua njia 19. Asiyekuwepo -na lake halipo 20. Asiyekuwepo machoni-na moyoni hayupo 21. Kuteleza-si kuanguka 22. Kipenda roho-hula nyama mbichi 23. Dunia mti mkavu-kiumbe usiuelemee 24. Mchagua jembe-si mkulima 25. Akipenda chongo-huita kengeza 26. Ng’ombe wa masikini -hazai 27. Mtakacha uvunguni-sharti ainame 28. Kutangulia-si kufika 29. Baniani mbaya -kiatu chake dawa 30. Asiyekujua -hakuthamini 31. Akutendaye mtende-mche asiye kutenda 32. Hakuna masika -yasiyokuwa na mbu 0688 821 584 George Kunguz - 3 33. Aibu ya maiti aijuaye mwosha 35. Mwenye chake-ni mungwana 36. Asiyekubali kushindwa – si mshindani 37. Akutukanaye-hakuchagulii tusi 38. Mbio za sakafuni-huishia ukingoni 39. Penye wengi-pana mengi 40. Mpiga ngumi ukutani-huumiza mkonowe 41. Aisifuye mvua-imemnyea 42. Mgaaga na upwa-hali wali mkavu 43. Penye nia – pana njia 44.Akufaaye kwa dhiki – ndiye rafiki wa kweli 45.Kikulacho -kinguoni mwako 46. Haba na haba--hujaza kibaba 47. Jungu kuu – halikosi ukoko 48. Mavi ya kale -hayanuki 49. Si vyote ving’aavyo - ni dhahabu 50.Aungurumapo simba-mcheza nani? 51. Alisifuye jua -limemwangaza 52. Akili nyingi-huondoa maarifa 53. Chelewachelewa-utakuta mwana si wako 54.Cha mtu mavi – ukikiona kiteme 55. Lakuvunda – halina ubani 56.Mficha uchi -hazai 57. Cha mlevi-huliwa na mgema 58.Kheri nusu shari-kuliko shari kamili 59. Mwenye macho-haambiwi tazama 60. Fimbo iliyo mkononi-ndiyo iuwayo nyoka 61. Akunyimaye kunde – kakupunguzia mashuzi 62.Fuata nyuki – ule asali 63. Chombo cha kuzama-hakina usukani 64.Chanda chema -huvikwa pete 65. Shukrani ya punda-ni mateke 66. Ukiiga kunya kwa tembo – utapasuka msamba 0688 821 584 George Kunguz - 4 67.Dua la kuku - halimpati mwewe 68. Wapishi wengi-huaribu mchuzi 69.Mchele mmoja -mapishi mbalimbali 70. Bora kufa moyo – kuliko kufa macho 71. Umoja ni nguvu -utengano ni udhaifu 72.Usipo ziba ufa - utajenga ukuta 73. Mama wa kambo-ni mama 74. Baba wa kambo - si baba 75. Dau la mnyonge — haliendi joshi 76. Barua ni -nusu ya kuonana 77. Fahari ya macho – haifilisi duka 78. Choko mchokoe pweza – binadamu hutamuweza 79.Dawa ya moto -ni moto 80. Bora kinga - kuliko tiba 81.Baada ya dhiki- faraja 82. Fimbo ya mbali - haiui nyoka 83.Chaka la simba — halali nguruwe 84. Nazi mbovu – haramu ya nzima 85.Dunia hadaa – ulimwengu shujaa 86.Bendera hufuata- upepo 87.Aliye kando-haangukiwi mti 88.Avumaye baharini papa-kumbe wengi wapo 89.Chako ulichokula leo-cha kesho cha mchimba kaburi 90.Amani haipatikani-bali kwa ncha ya upanga 91 .Mfa maji- haachi kutapatapa 92. Fumbo mfumbie mjinga- mwerevu ataling’amua 93. Gada la mua la jana-chungu kaona kivuno 94. Kipya kinyemi – ingawa kidonda 95. Kheri kenda shika-kuliko kumi nenda rudi 96.Kidole kimoja-hakivunji chawa 97. Zimwi likujualo – halikuli likakwisha 98.Kama hujui kufa-chungulia kaburi 99.Ukiona zinduna-ambari iko nyuma 0688 821 584 George Kunguz - 5 100. Hasira ya mkizi-furaha ya mvuvi 101.Undugu kufaana-sio kufanana 102. Meno ya mbwa-hayaumani 103. Fahari mawili -hawakai zizi moja 104.Donda ndugu — humaliza dawa 105. Jogoo la shamba-haliwiki mjini 106. Kimya kingi-kina mshindo mkuu 107.Kheri kujikwaa kidole-kuliko ulimi 108. Jino la pembe-siyo dawa ya pengo 109. Hatua ndefu – hufupisha mwendo 110. Embe dogo-ni dawa ya sukari 111.Gonga gogo -usikie mlio wake 112.Nguo ya kuazima-haisitili matako 113. Usiache mbachao -kwa msala upitao 114. Mtegemea cha nduguye – hufa masikini 115.Kinyozi - hajinyoi 116.Ila ya kikwapa – kunuka pasipo kidonda 117.Imara ya jembe-kaingojee shambani 118.Njia mbili – zilimshinda fisi 119. Kujikwaa siyo kuanguka-bali kwenda mbele 120.kheri atakula na nini-kuliko atakula nini 121.Ivumayo-haidumu 122.Kelele za chura- hazimzuii ng’ombe kunywa maji 123. Kanga – hazai ugenini 124 . Jifya moja-haliinjiki chungu 125.Kutoa ni moyo-usambe ni utajiri 126.Kizuri chajiuza -kibaya chajitembeza 127. Kulea mimba si kazi-kazi kulea mwana 128.kuvuja kwa pakacha – nafuu ya mchukuzi 129.Kiburi -si maungwana 130. Lake mtu halimtapishi – bali kumchefua 131.Kwenye miti-hakuna wajenzi 132.Akumulikaye mchana – usiku akakuchoma 0688 821 584 George Kunguz - 6 133. Kitanda usicho kilalia-hujui kunguni wake 134. Pema usijapo pema-ukipema si pema tena 135.Mali bila daftari – huisha bila habari 136. Macho – hayana pazia 137.Lila na fila-havitengamani 138.Maiti-haulizwi sanda 139. Kawaida ni kama sheria 140.Ulimi hauna – mfupa 141.Hakuna mjinga-akalipwa ziro 142. Elimu -ni bahari 143. Lisilo na mkoma-hujikoma lilo 144.Mbiu ya mgambo-ikilia kuna jambo 145.Masikini akipata-matako hulia mbwata 146.Manahodha wengi-chombo huenda mrama 147. Kwa mwoga huenda kicheko-kwa shujaa huenda kilio 148.Maneno mazuri-humtoa nyoka pangoni 149.Maji usiyoyafika – hujui wingi wake 150.Nzi kutua kwenye kidonda-si haramu 151. Maji yakimwagika-hayazoleki 152. Ndege mjanja-hunaswa na tundu bovu 153.Hakuna msiba-usio na mwenzake 154.Mjinga akielevuka – mwerevu yupo mashakani 156. Mshikwa na ngozi-ndiye mwizi 157.Bora anayekupandia chakula – kuliko anayekupa chakula 158. Mgomba haushindwi – na mkungu wake 159. Mkamia maji – hayanywi 160. Hakuna mchele-usio na chuya 161.Kunguru mwoga hukimbiza ubawa wake 162. Muuza sanda – mauti kwake harusi 163. Mchawi-mpe mtoto wako akulele 165. Ukistajabu ya musa – utaona ya filauni 166.Mwenye nguvu-mpishe 167. Aliyeshiba-hamjui njaa 0688 821 584 George Kunguz - 7 168. Usitukane wakunga ungali -uzazi ungalipo 169. Mkuki kwa nguruwe -kwa binadamu mchungu 170. Mtaka nyingi nasaba-hupa mingi misiba 171. Wagombanao – ndio wapatanao 172. Upele humwota – asiye na kucha 173. Usisahau u bahari – kwa sababu ya unahodha 174. Ukitaka kula nguruwe-chagua aliye nona 175. Teke la kuku-halimwumizi mwanaye 176. ukimona moshi-chini kuna moto 177. Shibe mwana malevya – njaa mwana malegeza 178 Penye urembo-ndipo penye urimbo 179. Ndugu wakigombana-chukua jembe ukalime 180. Samaki mkunje-angali mbichi 181. Waarabu wa pemba – hujuana kwa vilemba 182.Simba mwenda pole-ndiye mla nyama 183. Ukiona vyaelea-ujue vimeundwa 184. Anayekataa la wengi – ni mchawi 185. Aonjae asali-huchonga mzinga 186. Baada ya kisa mkasa-baada ya chanzo kitendo 187. Bora lawama – kuliko hasara 188. Debe tupu – haliachi kuvuma 189. Hapana siri-ya watu wawili 190.Hayawi hayawi – yamekuwa 191.Hisani – haiozi 192. Kata pua – uunge wajihi 193.Jogoo hulia-uta wangu ukule 194.kila chombo-na wimbile 195.Kisebusebu-na kiroho papo 196. Kupanda mchongoma-kushuka ndio ngoma 197.Kukopa harusi-kulipa matanga 198.Kuchamba kwingi-kuondoka na mavi 199.Masikini haokoti-akiokota huambiwa kaiba 200.Maji ya kifuu-bahari ya chungu 0688 821 584 George Kunguz - 8 201.liandikwalo-ndilo liwalo 202.Kumla nguruwe si kazi-kazi kumwosha 203.Bura yangu – sibadili na rehani 204. Wastara hazumbuki – wambili havai moja NAHAU 1. Fedha kichele – fedha kidogo 2. Shingo upande-kukubali pasipo hiari ya moyo 3. kuwa na mkono mrefu-kuwa mwizi 4. Ndumila kuwili-mnafiki 5. kuaga ukapera-kuoa 6. kifungua mimba-mtoto wa kwanza kuzaliwa 7. kufunga virago – kuondoka 8. Ana mranda baba yake-anafanana sana nababa yake 9. kupiga domo-mazungumzo marefu 10. Kuvimba kichwa – kuwa na kiburi 11. kufumba na kufumbua-haraka iwezekanavyo 12.kuwa na ulimi wa upanga-kuwa na maneno makali 13. Ndege mbaya-bahati mbaya 14. Ndege mzuri-bahati nzuri 15. Elimu ni bahari-elimu haina mwisho 16.Kupata cha mtema kuni-kupata mateso au taabu 17. kushika miguu-kuomba radhi 18. kuchanja mbuga-kwenda mbali 19. kufa kikondoo -kufa bila kitu 20. Kukata kamba-kufa 21. kupiga moyo konde-kuvumilia hadi mwisho 22. Kumchezea mtu shere-kumdhihaki 23. Kiguu na njia-hakai akatulia 24. Kufaa kishujaa-kufa kwa ajili ya wengine 25. Kufunga pingu za maisha-kufunga ndoa 26. Chemsha bongo-fikiri kwa makini 27. Kukata roho-kufa 0688 821 584 George Kunguz - 9 28. Kukata kiu-kumaliza hamu 29. Kuvalia njuga-kuingilia jambo lisilo kuhusu 30. kukata kona-kutoweka. 31. kuponda mali-kutumia mali kwa fujo 32. kuvaa miwani-kulewa pombe 33. kuaga dunia-kufa 34. kupiga maji-kulewa pombe 35. Kupiga mtindi-kulewa pombe 36. Kukata shauri-kuamua 37. Kumwekea mtu fundo-kukusudia kulipa kisasi 38. Chanda na pete-marafiki wa karibu 39. Kuchungulia kaburi-kuugua kukaribia kufa 40. Ashakhum si matusi-nisamehe kwa haya nitakayotamka 41. Mtahiniwa-mlengwa 42. Kupiga mbizi-kuogelea 43. kuzunguka mbuyu-kutoa au kupokea rushwa 44. Kwa udi na uvumba-kwa juhudi zote 45. kupiga mbiu-kutoa matangazo 46. Kuvika kilemba cha ukoka-kumsifia mtu sifa asizo stahili 47. Kupiga yowe-kupiga kelele kwa kuomba msaada 48. Kumkalia mtu kitako- kumseng’enya 49. Kupiga kibirizi-kutangaza jambo 50. Kuruka jiko-kuoa (kupata mke) 51. Kusimama kidete-kukazania jambo hadi mwisho 52. Kuzuga-kudanganya 53. Kububujika maneno-kupayuka maneno 54. Kupaka mafuta kwa mgongo wa chupa-kudanganya 55. Hawapikiki chungu kimoja – hawapatani kabisa 56. Ana kwa ana – uso kwa uso 57. Kuchora boya-kuunda njama za wizi 58. Mtoto wa kikopo – mhuni 59. Kujitia kitanzi-kijitia matatizoni 60. Kula jiwe-kunyamaza 0688 821 584 George Kunguz - 10 61. Kuwa na tumbo joto-kuwa na wasiwasi 62. Fuata giza-tii sheria 63. Kufyata mkia-kunyamaza kimya 64. Kukaa chonjo-kuwa na tahadhari 65. Kukata kauli-kuacha kusema 66. Kukata maini-kuumiza kwa kukatisha tamaa 67. Kukenua meno-kutoa meno nje 68. Kuangua kicheko-kucheka kwa sauti ya juu 69. Kuchochea utambi-kuchochea ugomvi 70. Kuezeka makofi-kupiga makofi 71. Kuchapa mguu-kutembea kwa mguu 72. kufanya juu chini-kufanya kila njia 73. Kumchimba mtu-kutafuta undani wa jambo kwa mtu 74. Enda chafya — kupiga chafya 75. Kuchanganya ulimi-kusema sana 76. kuanika meno — kucheka 77. Kupiga jeki – kutoa msaada 78. Utalijua jiji – shauri yako 79. Ona haya – ona aibu 80. Kutia chumvi – kuongeza maneno ya uongo 81. Hana mbele wala nyuma – hana chochote 82. Omba radhi – omba msamaha 83. Usiwe nyang’au – usidhurumu 84. Ana ndimi mbili – kigeugeu 85. Ana mkono wa birika – mchoyo 86. Akina pangu pakavu tia mchuzi – wafitini 87. Kujikaza kisabuni – kuvumilia 88. Kuandika meza – kuweka chakula mezani 89. Kushika tama – kushika shavu kwa huzuni 90. Kula mwande – kukosa ulichokusudia 91. Buheri wa afya – kuwa na afya njema 92. Kuvunjika moyo – kukata tamaa 93. Kujipalia mkaa – kujitia matatizoni 0688 821 584 George Kunguz - 11 94. Fuata nyayo – iga matendo 95. Kula chumvi nyingi – kuishi miaka mingi 96. Kutoa roho – kuua 97. Kupata jiko – kuoa au kuolewa 98. Bega kwa bega – kufanya jambo kwa ushirikiano 99. Kuwa macho – kuwa mwangalifu 100. Kuunga mkono – kukubali jambo Fulani 101. Kumeza mate – kutamani 102. Kulamba kisogo – kudharau yaliyo semwa 103. Kitinda mimba – mtoto wa mwisho kuzaliwa 104. Tega sikio – sikiliza kwa makini 105. Fuja mali – tumia mali ovyo 106. Andunje - mtu mfupi 107. Kula unga – kupata kazi 108. Kumwaga unga – kuachishwa kazi 109. Jitu la miraba minne – mtu mnene sana 110. Kupiga vigeregere - kushangilia VITENDAWILI 1. Bibi kizee amejitwika machicha-mvi 2. Mzazi ana miguu lakini mzaliwa hana miguu-kuku na yai 3. Ni mchoraji mzuri lakini hajui anachora nini-konokono 4. Ndugu yangu hata umchangieje haridhiki-tumbo 5. Tunatembea pamoja lakini mbona huongei?-kivuli 6. Kila ninapompiga mwanangu watu hucheza-ngoma 7. Rafiki yangu akitembea huringa hata akiwa hatarinikinyonga 8. Amefika kabla mjumbe hajarudi-mkwezi na nazi 9. Niliona cheni njiani lakini sikuweza kuinyanyua-siafu 10. Shamba langu kubwa lakini mavuno machache-nywele 11. Sijui anakokwenda wala anakotoka-upepo 12. Nimepigwa faini lakini kosa silijui – kujikwaa 13. Kuku wangu ana nyama ndanina mifupa nje-mua 14. Nimeona ng’ombe katika kundi la ndama -mwezi na nyota 0688 821 584 George Kunguz - 12 15. Askari wangu jasiri anapanda mlima-vidole na ugali 16. Mwanangu nikimkata hakatiki-maji 17. Huku ng’o na huko ng’o– giza 18. Wafu wanakokotana-jahazi na tanga 19. Tukutanapo ni marafiki,tuachanapo ni maadui-kinyesi 20. Kila ukiwaona wamejiandaa kupigana-katani 21. Nyumba yangu ndani kokoto nje simenti – pera 22. Mwanangu mvivu hawezi kupanda mlima-maji 23. Saa ya babu haijasimama tangu itiwe ufunguo-moyo 24. Nyumba yetu ina nguzo moja-uyoga 25. Kila nikikutana na adui yangu nanyong’onyea— ugonjwa 26.Gari langu halitumii mafuta ya waarabu-miguu 27.Jinamizi laniita lakini silioni-mwangwi 28 . Babu na bibi wana watoto sitini-saa 29. Nzi hatui juu ya damu ya simba-moto 30.Nina rafiki yangu kipenzi lakini namwogopa sana-kifo 31 .Wavu wangu haufai hata kuvulia samaki-utando wa buibui 32.Wakikua mama yao huwatupa mbali kwa kishindo-mbarika 33.Anauawa na uzazi wake-kinyonga,konokono 34.Mama hachoki kunibeba-kitanda 35.Mtoto wangu analia msituni-shoka 36. Watoto wa mfalme ni wepesi kujificha-macho 37.Nimeona bomu la machozi baridi-moshi 38.Ninapo mchapa mwanangu huwa nalia mwenyewe – kitunguu 39.Anaye nichoma sindano siyo dakitari wala tabibu-mbu 40.Wanangu watano kofia zinafanana - kucha 41.Wanangu utawaona wamevaa vizibao,wasiovaa si wanangu – kunguru wenye mabaka 42. Askari wangu mpole lakini adui wanamhara-paka 43.Kilio chake kwetu kicheko-mvua 44.Hesabu yake haina faida-nywele,mchanga,nyota 45.Namsikia lakini simuoni-sauti 46.Tangu nimemwosha mwanangu hakauki-ulimi 0688 821 584 George Kunguz - 13 47.Mbwa mwitu wamezunguka kumlinda-ulimi na meno 48.Visu vingi lakini mpini mmoja-chane za ndizi 49.Anajenga lakini hana mikono-ndege 50.Nilimch inja ng’ombe wangu tukala nyama,nikapanda mkia ukaota akawa ng’ombe mzima -mua 51.Ukoo wetu hauishiwi na safari-siafu 52.Huchagui wala hushauriwi – kuzaliwa na kufa 53.Mti wangu mkubwa sana umerundika ndege-shule 54.Ukiwagusa wanangu mimi hucheka-kwapa 55.Aliwa yuala, ala aliwa-nyangumi 56.Ubwabwa wa mwanangu mtamu-usingizi 57.Zoezi la kifo-usingizi 58.Kabla hajanitazama nishampiga-kujikwaa 58.Kabla hajanitazama nishampiga-kujikwa 59.Viti vyote vimekaliwa isipokuwa hicho-moto 60.Ziwa dogo linaruhusu mchanga-chungu jikoni 61.Wajukuu zangu wameshikana mpaka mwisho-mkufu 62.Wasio na uhakika wa sura zao humwendea-kioo 62.Watatu watatu ndio umoja wao – mafiga 63.Kila nikimsogelea naye husogea-kivuli 64.Askari wachapakazi hodari hawadai mshahara-nyuki 65.Ukinidharau utajutia-mwamba 66.Rafiki yangu mpendwa haniachi hata nikifa-sanda 67.Tochi yangu haitumii betri – jicho 68.Mchumaji hakula,mlaji hakumeza,mmezaji hakushiba-mikono, mdomo , koo 69.Tochi yetu huwaka mchana tu – jua 70.Mkwe wangu siwezi kumtazama machoni kwa mda mrefu-jua 71.Akienda kwa mjomba harudi-jani la mti 72.Watoto wa tajiri wa nguo lakini wanalala chini-boga 73.Athumani kapuku hupanda gari bure-nzi 74.Hana adabu wala staha kwa watu — utelezi 75.Maskini huyu habagui wala hachagui-kifo 0688 821 584 George Kunguz - 14 76.Nyumba yangu haina mlango-yai 77.Wanangu watatu akitoka mmoja walobaki hawafanyi kazimafiga 78 Tupo pamoja lakini hanifai kwa chochote hata niwapo hatarini – kivuli 79.Mwanangu mkaidi hainuki hata ukimwagiza kitu gani-maiti 80.Kamba yangu ni ndefu lakini haiwezi kufunga kuni-njia 81.Nimefagia uwanja wangu akaja miguu mirefu akautibuamvua 82.Nguo zangu hazichuji wala kupauka-maua 83.Kiwanja changu kinatembea-mtu mwenye kipara 84.Kuku wangu haatamii mayai yake-samaki 85.Mvua inanyesha ndani maji yanatiririka nje-kamasi 86.kiota changu kimezungukwa na boma la nyasi – macho 87.Gumugumu huzaa teketeke, teketeke huzaa gumugumu – mhindi 88.Hiki ndicho chakula kikuu cha mtoto-usingizi 89.Bibi hatui mzingo wake-konokono 90.Mzee huyu anakazi milele,asubuhi na jioni-ufagio 91.kuku wangu katagia mwibani- nanasi 92. Chemichemi yangu haikauki-mate 93.Kidonda hiki hatui nzi-moto 94.Unanitazama umenikuta? -kujikwaa 95. Kila mtu humwabudu-mlango. VISAWE VISAWE – Ni maneno tofauti lakini yenye maana sawa. 1. Marafiki=Maswahiba 2. Mtima =Moyo 3. Fujo =Gasia /vurugu 4. Chakula =Mlo 5. Tembo =Ndovu 6. Kifutio =Raba 7. Majira =Msimu 8. Kinywa =Mdomo 9. Familia =Kaya 0688 821 584 George Kunguz - 15 10. Utajiri =Ukwasi 11. Uso =Sura 12. Barua =Waraka 13. Jeuri =Kaidi 14. Tandiko =Godoro 15. Pombe =Mtindi 16. Jimbi =Jogoo 17. Labda =huenda 18. Juma =Wiki 19. Runinga =Televisheni 20. Sherehe =Tafrija 21. Vizuri =Vema 22. Shambulizi =Vamizi 23. Ajenti =Wakala 24. Duara =Mviringo 25. Msichana =Binti 26. Masikini =Fukara 27. Maradhi =Magonjwa 28. Mabaki =Masalia 29. Hawala =Kimada 30. Cheti =Hati 31. Kusudi =Azima 32.Munyu =Chumvi 33. Bahili =Mchoyo 34.Weka =Tia 35. Gari =Motokaa 36. Laghai =Danganya 37.Dua =Sala 38. Jasiri =Shujaa 39. Bibi =Nyanya 40.Chuo =Ndoa 41.Hisabati= Hesabu 42.Ukata =Umasikini 0688 821 584 George Kunguz - 16 43.Nepi =Winda 44.Tumbili= Ngedere 45. Vigelegele= Vifijo 46.Kumi na mbili= Thenashara 47. Tisa =Kenda 48.Pombe= Kileo 49.Wakati =Majira 50. Soka =Kandanda 51.Ruhusa =Idhini 52.Bingwa =Hodari9 53.Mola =Rabana 54.Kopoa =Zaa 55.Ulimi =Lisani 56.Ulimwengu =Dunia 57.Soni =Aibu 58.Hongo =Rushwa 59.Binadamu =Mtu 60. Mbogo =Nyati 61.Mvulana =Mvuli 62.Adha =Mateso 63.Hakika =Bayana 64.Angusha =Bwaga 65. Mwanzo =Awali 66. Punje =Chembe 67. Dhamira =Nia 68. Duni =Hafifu 69. Chukizo =Karaha 70. Karama =Kipawa 71. Sanamu =Kinyago 72. Kiango =Kinara 73. Kamwe =Kabisa 74. Riba =Faida 75. Nyara =Mateka 0688 821 584 George Kunguz - 17 76. Tafiti =Chunguza 77. kinyago =sanamu 78. Konde =Shamba 79. Kisulisuli =Chamchela 80. Uta =Upinde 81. Hadaa =Danganya 82. Muhula =Wakati/muda 83. Ishara =Dalili 84. Busara =Werevu/hekima 85. Eleza =Fafanua 86. Mafuriko =Gharika 87. Azimia =Kopesha 88. Chafya =Chemua 89. Hua =Njiwa 90. Funua =Kunjua 91. Maringo =Madaha 92. Matwa =Makapi 93. Raruka =Tatuka 94. Uwanja =Uga 95. Otea =vizia 96. Viungo =Via 97. Nuia =Kusudia 98. Utupu =Uchi 99. Elimu =Ujuzi 100.Panua =Tanua 101.Mkongonjo =Gongo/fimbo 102.Mjoli =Mtumwa 103.Tambua = Ng’amua 104. Mbari =Ukoo 105.Tetesi =Uvumi 106.Magugu =Nyasi 107.Kima =Bei 108.Vunda =Nuka 0688 821 584 George Kunguz - 18 Prepared by Sir Nyanda Meatu – Simiyu 2024